Ambwene Mwasongwe - Tumekubalika na Mungu mp3 Download

Ambwene Mwasongwe – Tumekubalika na Mungu mp3

Download mp3

Play Audio

Tumekubalika na Mungu Lyrics – Ambwene Mwasongwe

Loading…

About Song

TUMEKUBALIKA
Ni wimbo ambao Roho Mtakatifu alinipa mwaka 2018 nilipoitoa audio yake mwaka huohuo… na sasa namshukuru Mungu kwa kibali chake nimeweza kutoa video yake hii.

Nyuma ya ya wimbo huu Kuna Siri kubwa Sana ya Taifa la Israel ambalo mwaka 2018 lilikuwa linatimiza miaka 70 tangu warejee toka utawanyiko duniani kote mwaka 1948.

Israel ni taifa la Mungu kama yasemavyo maandiko matakatifu yaani Biblia. Na ni taifa limepitia vipindi vingi vizuri na vigumu….

Taifa hili limewahi Kaa utumwani Misri zaidi ya miaka 430, Mungu akalikumbuka likarejea chini ya Musa… baada ya Miaka 1500 Tena likaenda utumwani Babeli Israel (makabila 10 yakianza) Kisha Yuda (Makabila mawili)yakifuata miaka 130 baadaye…

lakini baada ya miaka 70 baadaye Mungu aliwarejesha lakini wakiwa Bado koloni la wamedi. kabla hawajapata uhuru wao.
Baadaye Warumi wakaja wakawatawala kwa miaka mingi, Kisha wakatawanywa duniani kote kwa muda wa miaka 1400+ mpaka waliporejea mwaka 1948 na kuwa Taifa tena.

Ndani ya miaka hii 70 wamekuwa wakitishwa sana na mataifa yaliwazunguka na msemo maarufu ni “Kuifuta Israel isiwepo juu ya uso wa Dunia”.

Siku moja nikiwa nafuatilia hotuba ya waziri wao mkuu akijibu hivyo vitisho, aliongea maneno mazuri na mazito ambayo ndiyo yaliamsha tafakari, na nilipoingia kuisoma Biblia Roho Mtakatifu akanisemesha kuhusu huu wimbo ukiwa umebebwa na maneno ya 1 Petro :2:9
Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

Maneno ya Waziri mkuu yaliyonigusa ni vile aliwakumbusha maadui zao kuwa wao Israel wanalindwa na kutunzwa na Mungu, Walisurvive Misri, Babeli na Walisurvive kutawanyika wakikumbwa na majaribio ya kuuwawa genocide nchi mbalimbali kwa sababu ya Yehova…

Akasema ni wao peke yao wamewahi shinda vita kwa nyimbo na mapambio, ni wao ambao wamekula chakula Cha mbinguni kilichodondoka jangwani, ni wao wamekunywa maji ya mwambani Tena jangwani, ni wao wamepona hatari ya magonjwa kwa mkono wa Mungu pasipo dawa, ni wao wamesafiri miaka 40 bila nguo na viatu kuchakaa…. na ni kwa sababu Moja kubwa ambayo Iko Zaburi 121:4

Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.

Kisha akauliza yako wapi mataifa yenye nguvu, wako wapi watawala wababe, yako wapi majeshi makubwa, yote yamepotea lakini Israel Bado yupo atakuwepo kwa sababu ya Mungu…

SASA ISRAEL NI PICHA YA MFANO WA KANISA… KWA SABABU HIYO TUNAYO KILA SABABU KUMWAMINI YESU NA KUISHI KWA UJASIRI NA USHINDI BILA KUJALI TUMEZUNGUKWA NA VITISHO GANI…

NAKUALIKA KUTAZAMA WIMBO HUU KWA JICHO NA SIKIO LA ROHONI ILI UWEZE KUHUDUMIWA NA ROHO MTAKATIFU ALIYENIHUDUMIA TANGU NAUANDAA MPAKA SASA…. USIACHE KUSHARE NA WENGINE USIACHE KUWATIA MOYO KWA BARAKA HIZI.

MUNGU AKUBARIKI SANA, NA KAZI YAKE IZIDI KUSONGA MBELE.

Ambwene Mwasongwe – Tumekubalika na Mungu mp3

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *